• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaeleza juhudi zake za kusaidia jamii ya kimataifa kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-11 17:56:17

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, wakati China inaendelea kufanya vizuri kazi za kukabiliana na maambukizi ya virusi vipya vya korona (COVID-19), inapenda kutoa mchango kwa mapambano dhidi ya ugonjwa huo duniani.

    Geng amesema hatua zitakazochukuliwa na China katika kusaidia jamii ya kimataifa kukabiliana na ugonjwa huo ni pamoja na kuongeza mawasiliano na uratibu na Shirika la Afya Duniani na jamii ya kimataifa, kubadilishana uzoefu na nchi nyingine duniani, kupeleka wataalamu kwa nchi zinazohitaji, kutoa misaada ya dawa na vifaa kwa jamii ya kimataifa, na kuongeza ushirikiano wa teknoljia za kisayansi na nchi nyingine.

    Geng amesema, China itashirikiana na jamii ya kimataifa kupata ushindi wa mwisho katika vita dhidi ya COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako