• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wapomgeza NEMC vita taka sumu

    (GMT+08:00) 2020-03-11 19:30:22

    BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limepongezwa na wadau kwa kupambana na taka zenye sumu ili zisitapakae nchini. Hayo yalibainishwa katika mkutano wa wafanyabiashara ambao walijadili, pamoja na mambo mengine, mafanikio na matatizo ya utekelezaji wa marufuku ya mifuko ya plastiki. Marufuku hiyo ilianza Juni 1, mwaka jana.

    Wajumbe walisema moja ya tatizo kubwa linaloikabili dunia ni namna ya kupambana na taka zenye sumu na taka za aina nyingine, ambazo huongezeka kwa wingi kila siku kwa sababu ya ongezeko la watu na shughuli zao.

    Baada ya kuliona hilo, Baraza hilo lilisisitiza kwamba kila kiwanda nchini kiwe na cheti cha tathmini ya athari kwa mazingira (TAM) na kufanya ukaguzi.

    Mbali ya cheti hicho, NEMC inafanya ukaguzi wa viwanda na maeneo ya biashara na kutoa elimu kwa umma.

    Mwishoni mwa wiki NEMC iliharamisha vifungashio vya tubing, ambavyo vinatumika kufungia karanga, barafu, korosho na ubuyu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako