• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwakilishi wa China atoa wito jamii ya kimataifa kusaidia Afrika kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2020-03-12 09:57:24

    Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun akizungumza kwenye mjadala wa baraza la Usalama la UN kuhusu kupambana na ugaidi na itikadi kali, amesisitiza kwamba jamii ya kimataifa inapaswa kuisaidia Afrika kupambana na ugaidi na itikadi kali kwa njia za pande zote.

    Balozi Zhang amesema ugaidi ni adui wa binadamu wote, bara la Afrika limeathiriwa sana na ugaidi na itikadi kali katika miaka ya hivi karibuni, ambalo inaendelea kuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugaidi, hivyo anaona jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua za haraka, madhubuti na za uratibu ili kuzisaidia nchi za Afrika kuongeza uwezo, rasilimali na hatua za kukabiliana tishio la ugaidi na itikadi kali.

    Aidha balozi Zhang amesema China iko tayari kufanya kazi na jumuiya ya kimataifa kuzisaidia nchi za Afrika kupambana na ugaidi na siasa kali na kuendelea kutekeleza jukumu katika kukuza amani, utulivu na maendeleo barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako