• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yasema watuhumiwa wa jaribio la kumuua waziri mkuu wamekamatwa

    (GMT+08:00) 2020-03-12 10:07:54

    Serikali ya Sudan imesema watuhumiwa waliohusika na jaribio la kumuua waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Abdalla Hamdok wamekamatwa.

    Waziri wa Habari wa Sudan ambaye pia ni msemaji wa serikali Bw. Faisal Mohamed Saleh, amesema watuhumiwa kadhaa wakiwa ni pamoja na wageni wamekamatwa. Akiongeza kuwa timu ya usalama ya Marekani jana ilifika Khartoum na kushirikiana na wapelelezi wa Sudan kufanya uchunguzi. Pia amedokeza kuwa mipango mipya imetekelezwa katika kulinda usalama wa nchi hiyo, na polisi na idara ya upelelezi zimechukua hatua kuhakikisha usalama wa waziri mkuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako