• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Danny Drinkwater kutemwa na Aston Villa baada ya kumpiga kichwa mwenzake mazoezini

  (GMT+08:00) 2020-03-12 12:11:29

  Klabu ya Aston Villa inatarajia kusitisha mkataba wake wa mkopo na Danny Drinkwater baada ya kiungo huyo kumpiga kichwa mwenzake Jota mazoeni. Villa ilimsajili kwa mkopo wa muda mrefu Drinkwater kutoka Chelsea, lakini kitendo chake cha kugombana mazoezini kimeifanya klabu hiyo kuamua kusitisha mapema mkataba huo. Drinkwater amecheza mechi nne tangu ajiunge Villa Januari katika mpango wa kuinusuru klabu hiyo na janga la kushuka daraja. Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinadai kuwa Drinkwater alimpiga kichwa Jota katika mazoezi ya juzi Jumanne na kuwatolea maneno makali wenzake. Tukio la kiungo huyo mwenye miaka 30 kupigana na kutoa maneno makali kwa wenzake limesababisha viongozi wa Villa Park kufikiria kukatisha mkataba wake haraka, lakini uamuzi wa mwisho kama arudishwe Chelsea bado haujawekwa wazi. Pia, anaweza kukutana na adhabu kali kutoka Villa ikiwamo kupigwa faini kubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako