• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasisitiza ari ya kuondoa umaskini kwa wakati uliopangwa licha ya athari ya COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-03-12 17:34:39

  Mkurugenzi wa ofisi ya kupambana na umasikini iliyo chini ya Baraza la Serikali la China Bw. Liu Yongfu leo amesema, baada ya juhudi za zaidi ya miaka minne, wilaya zenye umaskini uliokithiri nchini China imepungua na kufikia 52 kutoka 832 mwishoni mwa mwaka 2012. Amesisitiza kuwa, maambukizi ya COVID-19 hayataathiri vigezo, muda na kazi ya kuondoa umaskini, pia hayatabadilisha imani na nia ya China ya kutimiza lengo hilo kwa wakati uliopangwa.

  Serikali ya China iliweka lengo la kuondoa kabisa umaskini mwaka huu. Sasa zimebaki siku zisizozidi 300. Lakini maambukizi ya COVID-19 yameleta changamoto mpya, na kuathiri vibarua wanaotoka maeneo yenye umaskini kwenda nje kutafuta ajira, kuuza mazao ya kilimo na kutekeleza miradi ya kuwasaidia watu maskini.

  Bw. Liu Yongfu amesema, kutokana na kupungua kwa maambukizi ya COVID-19, na hatua husika zilizochukuliwa na serikali, athari ya maambukizi hayo inazidi kupungua.

  "Mwaka jana, idadi ya vibarua wanaotoka maeneo maskini wanaofanya kazi nje ni milioni 27.29, hadi tarehe 6 Machi watu milioni 14.2 wameondoka makwao. Katika wiki ya kuanzia tarehe 28 Februari hadi tarehe 6 Machi, idadi hiyo iliongezeka milioni 3. Tunakadiria kuwa idadi hiyo itaongezeka zaidi. Aidha, hadi tarehe 6 Machi, theluthi moja ya miradi ya kuwasaidia watu maskini imeanza kutekelezwa, na inaharakishwa zaidi. Hatubadilishi nia na imani yetu ya kutimiza malengo yetu kutokana na maambukizi. Tunapaswa kuendelea na malengo yetu na kuongeza nguvu za kutimiza malengo hayo. "

  Ofisa huyo amesema, baada ya juhudi za miaka zaidi 7, hasa katika miaka minne iliyopita toka serikali ya China ianzishe kampeni ya kuondokana na umaskini kabisa, idadi ya watu maskini vijijini imepungua na kufikia milioni 5.51 mwishoni mwa mwaka jana, kutoka watu milioni 98.99 mwishoni mwa mwaka 2012. Takwimu zinaonyesha kuwa lengo la kuondoa umasikini linakaribia kutimizwa.

  Bw. Liu pia amesema, katika watu zaidi milioni 93 walioondolewa umaskini, baadhi bado wako katika hali ya udhaifu wa kiuchumi, ni lazima kuzuia wasirudi kwenye umaskini. Pia kuna wengine ambao wako katika ukingo wa umaskini, kwa hiyo inapaswa kuwazuia wasiingie kwenye umaskini.

  "Kwa wale waliondolewa kwenye umaskini, kazi yetu muhimu ni kuendelea na hatua za hivi sasa, kama vile kuendeleza sekta zinazowajengea uwezo wa kujiendeleza, na kutoa nafasi za ajira. Vilevile kwa wale wako ukingoni mwa kuingia kwenye umaskini, tutajenga mfumo wa kuwafuatilia hali yao na kuwasaidia."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako