• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yasitisha safari zote za nchi za Ulaya kuingia Marekani isipokuwa Uingereza

    (GMT+08:00) 2020-03-12 18:38:13
    Marekani itasitisha safari zote kutoka nchi za Ulaya isipokuwa Uingereza kwa muda wa siku 30, ikiwa ni hatua mpya ya kukabiliana na maambukizi zaidi ya virusi vya korona (COVID-19).

    Rais wa nchi hiyo Donald Trump amesema jana usiku kuwa, vizuizi hivyo vitaanza kutekelezwa ijumaa usiku, na vitaweza kubadilishwa kutokana na mazingira yatakavyokuwa nchini humo. Rais huyo pia amewataka wananchi wake kuchukua tahadhari zote na kulitaka bunge kuchukua hatua zaidi za unafuu wa kodi.

    Rais Trump ameliomba bunge hilo kuongeza ufadhili kwa dola bilioni 50 zaidi ili kuunga mkono biashara ndogo zinazoathirika na mgogoro wa kiuchumi kutokana na mlipuko wa virusi vya korona. Rais Trump amesema, ameielekeza Idara ya Kusimamia Biashara Ndogo kuchukua mamlaka yake na kutoa mitaji kwa viwanda vilivyoathiriwa na virusi vya korona, ili kuunga mkono zaidi wafanyabiashara, familia na wafanyakazi nchini Marekani.

    Habari nyingine zinasema Umoja wa Ulaya leo umetangaza kuwa unapinga hatua ya Marekani ya kuzuia safari za nchi za Ulaya kuingia nchini Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako