• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Wakulima wa kilimo cha matunda na mboga walia ukosefu wa soko

    (GMT+08:00) 2020-03-12 18:44:36

    Rwanda ina mpango mkubwa wa kufanya kilimo cha mboga na matunda kuwa mojawapo ya sekta itakayosaidia kuongeza mapato ya mauzo ya nje ya nchi hiyo.

    Kulingana na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB) sekta hiyo hivi sasa inachangia asilimia 50 ya mauzo ya nje ambayo sio ya kawaida.

    Hata hivyo ,wakulima wanaojishughulisha na uzalishaji wa mboga na matunda wanasema kuwa ukosefu wa soko la kuaminika na endelevu unaendelea kuathiri kilimo cha matunda na mboga.

    Kulingana na mkulima Moussa Moustapha Musabyimana,kutoka eneo la Busasamana katika Wilaya ya Rubavu,wakulima wanakabiliwa na ukosefu wa soko,akielezea uzoefu wake akijaribu kuingia katika soko la ndani.

    Alisema wiki kadhaa zilizopita ,kwa msaada wa maafisa wa wilaya,walikwenda katika hoteli kadhaa katika wilaya ya Rubavu kujaribu kuwashawishi wanunue bidhaa zao ,na baada ya kupewa hakikisho,hawakusikia tena kutoka kwa hoteli hizo.

    Hoteli nyingi nchini Rwanda zinategemea mboga zinazoagizwa kutoka ukanda wa afrika mashariki,licha ya wakulima kuongeza uzalishaji na usambazaji katika soko la ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako