• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzoefu wa China waisaidia dunia kuepuka makosa katika kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-12 19:10:39

    Mtaalam wa mfumo wa hewa nchini China Zhong Nanshan amesema uzoefu wa China unaweza kuisaidia dunia kuepuka makosa katika kupambana na mlipuko wa virusi vya korona (COVID-19).

    Akizungumza na wanahabari mjini Guangzhou, Dokta Zhong amesema, kiwango cha vifo vinavyotokana na virusi vya korona katika nchi za nje ni sawa na ilivyokuwa katika siku za mwanzo mjini Wuhan. Amesema ni muhimu kuimarisha mawasiliano kati ya China na nchi na sehemu nyingine duniani, kwa kuwa uzoefu na mafunzo yaliyopatikana nchini China katika miezi miwili iliyopita vinaweza kusaidia dunia kupunguza kiwango cha maambukizi na vifo vinavyotokana na virusi hivyo.

    Ameongeza kuwa, kama nchi nyingine zinaweza kuchukua hatua kama zilizochukuliwa na China, janga la virusi vya korona duniani linaweza kudhibitiwa ifikapo Juni mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako