• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini na Algeria zaripoti kesi mpya za maambukizi ya virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-03-12 19:46:52

    Serikali ya Afrika Kusini imeripoti kesi nne mpya za maambukizi ya virusi vya korona ambapo idadi ya jumla ya wagonjwa wa COVID-19 nchini humo imefikia 17.

    Waziri wa afya nchini humo Bw. Zweli Mkhize amesema, kesi hizo nne ni pamoja na mtu mmoja aliyeambukizwa ndani ya nchi na wengine watatu walirejea nchini humo kutokea nchi za nje.

    Habari nyingine inasema, wizara ya afya nchini Algeria leo imetangaza kifo cha kwanza cha maambukizi ya virusi hivyo na kesi nyingine 5 mpya zilizogunduliwa katika mikoa ya Blida, Tizi Ouzou na Souk Ahras. Kutokana na kesi hizo, Algeria ina jumla ya kesi 24 ya virusi vya korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako