• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya wataalamu wa China wawasili Rome

    (GMT+08:00) 2020-03-13 09:29:58

    Ndege iliyobeba timu ya wataalamu 9 wa China na vifaa vya matibabu imewasili nchini Italia, ikiwa sehemu ya juhudi za China kuisaidia Italia kupambana na mlipuko wa virusi vya korona.

    Hii ni timu ya tatu ya wataalamu iliyotumwa na serikali ya China baada ya timu zilizotumwa Iran na Iraq.

    Habari nyingine zimesema, waziri wa mambo ya nje wa Tunisia Noureddine Erray amesema Tunisia inapenda kubadilishana na China uzoefu wa kupambana na maambukizi ya virusi vya korona.

    Alipokutana na balozi wa China nchini Tunisia Wang Wenbin, Bw. Erray amepongeza juhudi za serikali ya China na wananchi wake kupambana na virusi vya korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako