• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kocha wa Arsenal Mikel Arteta akutwa na virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-03-13 12:11:23

    Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amepimwa na kukutwa na virusi vya korona. Washika bunduki hao wamefunga uwanja wa mazoezi na wafanyakazi wote wa klabu ambao waliokutana na Arteta sasa watajiwekea karantini. Ligi ya Premier itafanya mkutano wa dharura leo kujadili mechi zake. Arsenal inategemea watu wake kadhaa muhimu kujiwekea karantini, kikiwemo kikosi kizima cha kwanza. Imefahamika kuwa kalabu zote 20 za Ligi ya Premier zinataka kuamua makakti mmoja, na njia moja ambayo inaweza kujadiliwa kwenye mkutano ni kuahirisha mechi zote 10 za wikiendi hii. Arsenal ilikuwa na ratiba ya kucheza kesho Jumamosi dhidi ya Brighton kwenye Ligi ya Premier lakini mechi imeahirishwa. Awali wachezaji kadhaa wa Arsenal walitengwa baada ya kubainika kwamba mmiliki wa klabu ya Olympiakos, Evangelous Marinakis ana virusi vya korona. Arsenal ililazimika kufanya hivyo baada ya kubaninika kwamba Marinakis mwenye umri wa miaka 52, alikutana na baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo ya EPL ilipochuana na Olympiakos katika mechi ya Europa League mnamo Februari 27, 2020, ugani Emirates.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako