• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ripoti ya ukiukwaji wa haki za binamu wa Marekani kwa mwaka 2019

  (GMT+08:00) 2020-03-13 17:01:06

  Yaliyomo

  Dibaji…………………..2

  Moja. Haki za kiraia na haki za kisiasa zipo katika maandishi tu……………..6

  Pili. Haki za kiuchumi na kijamii zinakosa ulinzi wa kimsingi……….12

  Tatu. Makundi ya watu walio wachache wananyanyaswa na kutengwa……..18

  Nne. Wanawake wanakabiliwa na ubaguzi mkali na mabavu…………..29

  Tano. Makundi ya watu wanyonge wanaishi kwa taabu…………………..34

  Sita. Wahamiaji wananyimwa haki zao za kimsingi…..40

  Saba. Kuingilia ovyo haki za binadamu za nchi nyingine…..45

   

  Dibaji

  Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alipotoa hotuba tarehe 15, Aprili, mwaka 2019, alisema "Tunasema uwongo, tunadanganya, tunaiba……. Huu ndio utukufu wa maendeleo ya Marekani."

  Kauli ya mwanasiana huyu wa Marekani imeonesha wazi unafiki wake wa kutumia vigezo viwili katika masuala ya haki za binadamu na kulinda umwamba kwa kisingizio cha haki za binadamu.

  Marekani inajigamba kuwa nchi inayojengwa katika msingi wa haki za binadamu na kujifanya kama ni mtetezi wa haki za binadamu duniani. Kwa kutumia uelewa mbaya juu ya haki za binadamu, na kutimiza lengo kuu la kuongoza dunia, kila mwaka Marekani inaandaa ripoti ya haki za binadamu ya nchi moja moja kwa mujibu wa taarifa zisizo na uhakika na uvumi, ambapo inapotosha na kudhalilisha hali ya haki za binadamu ya nchi na sehemu ambazo hazikidhi maslahi yake ya kimkakati, lakini inaziba masikio na kufumbia macho matukio mengi ya ukiukwaji mbaya wa haki za binadamu yanayotokea nchini humo.

  Data zilizonukuliwa kwenye ripoti hii zote zinatokana na takwimu, taarifa za habari na ripoti za utafiti zinazopatikana kwa umma. Yaliyomo katika ripoti hii ni ushahidi kuwa katika miaka ya hivi karibuni, haswa baada ya mwaka 2019, hali ya haki za binadamu nchini Marekani ni mbaya na inazidi kuzorota.

  -----------Marekani inaongoza duniani kwa matumizi mabaya zaidi nguvu, hasa ya kutumia bunduki. Mwaka 2019, nchi hiyo ilishuhudia mashambulizi makubwa 415 ya bunduki, sawa na kila siku zaidi ya tukio moja; watu 39,052 waliuawa kwenye matukio ya mabavu yanayohusiana na bunduki, sawa na kila dakika 15 mtu mmoja aliuawa kwa bunduki. Gazeti la US TODAY limetoa tahariri likisema, "pengine Marekani imeingia kwenye zama za ufyatuliaji risasi mbaya".

  -----------Uchaguzi umekuwa mchezo wa pesa wa matajiri. Mwaka 2018, matumizi kwenye uchaguzi wa katikati ya muhula yalifikia dola za kimarekani bilioni 5.7, na kuwa uchaguzi wa wabunge ulio ghali zaidi katika historia; Wafadhali binafsi wakubwa 10 walitoa dola za kimarekani milioni 436 kwa kamati ya utekelezaji wa kisiasa, maarufu kama Super PACS. Mashindano ya kukusanya fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 yanazidi kuwa makali, na wagombea wote wamepata zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1.08.

  ------------Pengo kati ya matajiri na maskini nchini Marekani ni kubwa zaidi miongoni mwa nchi zilizoendelea. Mwaka 2018, kipimo cha Gini kilifikia 0.485, na pengo kati ya matajiri na maskini liliweka rekodi mpya ya kihistoria. Asilimia 10 ya familia tajiri zaidi zinamiliki asilimia 75 ya utajiri wote nchini Marekani. Kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 2018, asilimia 50 ya familia maskini zaidi hazikupata ongezeko la utajiri.

  -----------Marekani ni nchi pekee iliyoendelea yenye mamilioni ya watu wanaokosa chakula. Takwimu za mwaka 2018 zilizotolewa na Idara ya Sensa ya Watu ya nchi hiyo zimeonesha kuwa Marekani ina watu maskini milioni 39.7. Kila usiku wamarekani wasiopungua laki 5 hawana sehemu za kulala. Watu milioni 65 wanakosa tiba kutokana na gharama kubwa ya matibabu.

  ----------Uhalifu unaotokana na ubaguzi na chuki nchini Marekani unashangaza dunia. Wimbi la mamlaka ya watu weupe linarudi, na matukio mengi ya kigaidi yaliyotokea nchini humo katika miaka ya karibuni yalihusiana na matumizi ya nguvu yaliyochochewa na mamlaka ya watu weupe. Watu 22 waliuawa katika shambulizi la bunduki katika duka la Wallmart mjini El Paso, na sababu ya mshambuliaji mweupe kufanya hivyo ni chuki dhidi ya watu wa Latin Amerika. Uchambuzi unasema, "Marekani siku zote iko katika msukosuko wa ugaidi wa mamlaka ya watu weupe."

  ----------Matukio ya polisi kuwaua kwa risasi na kuwatesa wamarekani wenye asili ya kiafrika yanatokea mara kwa mara. Kiwango cha kufungwa jela kwa watu wazima wenye asili ya kiafrika ni mara 5.9 zaidi ya kile ya watu wazima weupe. Mtoa ripoti maalum wa Umoja wa Mataifa amesema kufungwa jela kwa watu wengi namna hiyo ni sumu inayobaki ya utumwa na kutengwa kwa watu wa rangi tofauti.

  -----------Pengo kati ya watu wa rangi tofauti katika ajira na utajiri ni kubwa kiasi cha kutisha. Katika miaka 40 iliyopita, kiwango cha ukosefu wa ajira cha wafanyakazi wenye asili ya kiafrika ni mara mbili kuliko kile cha watu weupe. Utajiri wa wastani wa familia ya watu weupe ni mara 10 zaidi ya familia ya watu weusi. Kwa mujibu wa hali ya sasa, itachukua miaka zaidi ya 200 kwa familia za watu weusi kupata utajiri walio nao sasa familia za watu weupe.

  -----------Ukosefu wa uvumilivu kwa dini unaendelea kuzorota. Utafiti uliofanywa na Kituo cha Utafiti cha Pew umeonesha kuwa asilimia 82 ya watu waliohojiwa wanaona waislamu wanakabiliwa na unyanyapaa, na asilimia 64 ya watu waliohojiwa wanaona wayahudi wanakabiliwa na unyanyapaa nchini Marekani. Mwaka 2018, watu wenye msimamo mkali walifanya matukio 249 dhidi ya wayahudi. Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaona kuwa matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya wayahudi yapo nchini Marekani.

  ----------Marekani ni nchi yenye kipato cha juu ambayo wanawake wanaishi kwenye hatari zaidi. Asilimia 92 ya wanawake wanaouawa kwa bunduki katika nchi zenye kipato cha juu wanatoka Marekani, na kiwango cha kuuawa kwa bunduki kwa wanawake nchini Marekani ni mara 21 zaidi kuliko nchi nyingine zenye kipato cha juu, kwa wastani kila mwezi wanawake 52 wanauawa na wapenzi wao. Asilimia 70 ya wanawake wa Marekani wanadhalilishwa kimwili na kingono na wapenzi wao.

  ----------Tatizo la umaskini wa watoto linatisha. Marekani bado ina watoto milioni 12.8 wanaoishi kwenye umaskini, na idadi ya watoto maskini wenye umri wa chini ya miaka mitano imefikia milioni 3.5, milioni 1.6 kati yao wakiwa wanaishi katika umaskini uliokithiri. Mfuko wa Ulinzi wa Watoto wa Marekani umekosoa kuwa "katika nchi tajiri zaidi duniani, kuna zaidi ya moja kwa tano ya watoto wanakabiliwa na hali ngumu kila siku, yaani nitakula nini chakula kinachofuata, nitalala wapi leo?"

  ----------Tatizo la umaskini wa wazee linazidi kuwa kubwa. Kati ya wazee wenye umri wa miaka zaidi ya 60 nchini Marekani, kila watu 12, kuna mmoja anakosa chakula cha kutosha, na idadi hiyo kwa jumla imefikia milioni 5.5. Asilimia 40 ya watu wa tabaka la kati wa Marekani wanakaribia na kuingia kwenye umaskini wanapofika umri wa miaka 65.

  ---------Sera ya serikali ya Marekani kwa wahamiaji inazidi kuwa kali na katili. Sera ya "kutovumilia hata kidogo" imesababisha watoto wengi kulazimika kuachana na familia zao. Toka mwezi Julai mwaka 2017, idara ya uhamiaji imewatenganisha watoto zaidi ya 5,400 na wazazi wao. Toka mwaka 2018, wahamiaji 24 wakiwemo watoto 7 wamekufa walipowekwa mbaroni katika kambi za hifadhi katika sehemu za mipakani za Marekani.

  ----------Marekani inajulikana kama "nchi ya kwanza inayopenda vita katika historia ya binadamu". Tangu mwaka 2001, Marekani haijasimamisha kuanzisha vita katika nchi na sehemu nyingine duniani, ambavyo vimeigharimu zaidi ya dola za kimarekani trilioni 6.4, kusababisha vifo vya watu zaidi ya laki 8 na mamilioni ya watu kupoteza makazi duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako