• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya Airways yasitisha safari zake kati ya Nairobi na Rome, Geneva

    (GMT+08:00) 2020-03-13 19:49:44

    Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways limesitisha safari zake kati ya Nairobi na Rome pamoja na Geneva kama njia ya kuzuia uwezekano wa kuenea kwa virusi vya korona.

    Shirika hilo limesema kwenye taarifa kwamba usitishaji huo unaanza kutekelezwa tarehe 13 Machi hadi 30 Aprili.

    Kenya imethibitisha tukio la kwanza la korona Ijumaa na tayari serikali imetangaza hatua kadhaa za kuikabili ikiwa ni pamoja na kufuta mikutano yote na kupunguza safari za nje ya nchi.

    Kenya Airways imesema inaendelea kudumisha ukaguzi na usafi wa hali ya juu kwa wafanya kazi na wasafiri wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako