• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Mradi wa umwagiliaji wasaidia wakulima wilaya ya Kirehe

    (GMT+08:00) 2020-03-13 19:50:11
    Mradi wa umwagiliaji wa Nasho chini Rwanda ambao ni uwekezaji wa pamoja wa Serikali ya Rwanda na wakfu wa Howard G. Buffett , umeongeza pakubwa mavuno katika eneo hilo na hivyo kuongeza mapato yao.

    Mradi huo ulianzishwa ili kuboresha kilimo cha kisasa nchini Rwanda na kuboresha zaidi maisha wakulima wadogo.

    Kwa jumla Mradi huo una mifumo 73 ya kumwagilia maji kwenye eneo la hekta 1,173 na kunufaisha wakulima 2,099 wadogo.

    Akizindua mradi huo rasmi rais Paul Kagame amesema kuunganisha kilimo na uhifadhi kumeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya wakaazi ambao awali walitegemea misaada tu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako