• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa afya wa kanda ya Afrika ya Kati wakubaliana kuongeza mapambano dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-13 20:21:27

    Mawaziri wa Afya kutoka nchi za Afrika ya Kati wamekubaliana kupambana kwa pamoja dhidi ya virusi vya korona (COVID-19) na kubadilishana taarifa na hatua sahihi.

    Nchi sita wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi na Fedha ya Afrika ya Kati (CEMAC) wametoa ahadi hiyo baada ya mkutano wao kuhusu virusi vya korona uliofanyika katika mji mkuu wa Cameroon, Douala.

    Waziri wa Afya wa Cameroon Manaouda Malachie aliyeongoza mkutano huo amesema, mawaziri hao wamesisitiza ushirikiano wa dharura kuhusu ufuatiliaji, kuzuia, kugundua na kudhibiti wa virusi vya korona katika kanda hiyo.

    Mpaka sasa, nchi za Cameroon na Gabon zimeripoti kuwa na kesi za maambukizi ya virusi vya korona katika kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako