• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kasi ya ukuaji wa uchumi wa Afrika yatarajiwa kushuka na kuwa asilimia 2 mwaka huu

    (GMT+08:00) 2020-03-15 19:20:44

    Katibu mtendaji wa Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa Bibi Vera Songwe amesema, kasi ya ukuaji wa uchumi wa Afrika inaweza kushuka na kuwa asilimia 2 kutoka asilimia 3.2 iliyotarajiwa zamani.

    Bibi Songwe amesema hayo kwenye mkutano na wanahabari kuhusu athari ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa uchumi wa Afrika. Amesema kutokana na ugonjwa huo, mwaka huu, mapato ya mauzo ya mafuta ya Afrika yatapungua kwa dola bilioni 101 za Kimarekani, licha ya hayo, ugonjwa huo pia utasababisha hasara kubwa kwa sekta ya utalii, na kupungua kwa uwekezaji wa nje na uwekezaji wa ndani.

    Aidha, amesema Afrika pia itatumia dola bilioni 10.6 za Kimarekani katika kukabiliana na COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako