• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa yasema COVID-19 kuigharimu Afrika mabilioni ya dola

    (GMT+08:00) 2020-03-15 19:31:24

    Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa UNECA imesema msukosuko wa virusi vya Korona unaweza kuigharimu Afrika mabilioni ya dola ya mapato ya uuzaji nje wa bidhaa.

    Katibu Mkuu mtendaji wa UNECA Bibi Vera Songwe, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa, taarifa ya UNECA inaonyesha kuwa virusi vya Korona bila shaka vinaathiri biashara barani Afrika. Amesema Afrika inaweza kupoteza nusu ya GDP, na ongezeko lake linaweza kupungua kutoka asilimia 3.2 ya sasa hadi asilimia mbili.

    Bibi Songwe amesema hayo wakati nchi mbalimbali za Afrika zinaendelea kushuhudia watu wakiambukuzwa virusi vya Korona. Nchini Kenya tayari mtu wa kwanza ameripotiwa kuambukizwa virusi vya Korona, lakini sasa hali yake ni tulivu. Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza raia wa Italia aliyeingia nchini humo kuambukizwa virusi ya Korona.

    Nchini Rwanda wizara ya afya ya nchi hiyo imewataka watu wake kuwa makini na watulivu, kufuatia mtu mmoja kugunduliwa na virusi vya Korona. Sudan imeamua kufunga vyuo na shule kufuatia mtu mmoja kufa kutokana na virusi vya Korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako