• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Wachezaji wa Gremio waingia uwanjani wakivaa mask wakipinga mechi dhidi ya Sao Luiz

  (GMT+08:00) 2020-03-16 08:38:41

  Wachezaji kutoka klabu ya Gremio ya Brazili jana waliamua kuingia kiwanjani wakiwa wamevaa mask ili kupinga amri ya kucheza mechi ya soka huku hofu ikitanda juu ya kuongezeka kwa virusi vya korona nchini humo. Wachezaji, wakiongozwa na kocha wao Renato Portaluppi, walitoka kwenye vyumba vya kubadili nguo na kuingia uwanjani huku wakiwa wamevaa mask na kujipanga kabla ya mchezo dhidi ya Sao Luiz kuanza. Hakuna shabiki aliyeruhusiwa kuingia kutazama mechi hiyo iliyopigwa katika kiwanja cha Gremio Arena, ambapo Gremio ilishinda 3-2 wakiwa hawajavaa tena mask wakati wa mechi. Baada ya mechi Portaluppi amesema ulimwengu mzima umesimama na soka ya Brazil pia inapaswa kuismama pia. Pingamizi hiyo imekuja huku wachezaji na klabu za nchi hiyo wakianza kulalamikia uamuzi uliotolewa na mamlaka za soka wa kuamuru mechi zichezwe bila ya watazamaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako