• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KASHFA: Ukad kufanya uchunguzi mpya juu ya madai ya mkulima ya nyama aliyopewa Furry

    (GMT+08:00) 2020-03-16 08:39:07

    Mamlaka inayopambana na dawa zilizopigwa marufuku michezoni ya Uingereza Ukad, inapanga kuchunguza madai ya mkulima Martin Carefoot aliyeambiwa adanganye ili kusaidia kesi ya bingwa wa ndondi duniani Tyson Fury. Fury na binamu yake Hughie waligundulika kutumia dawa zilizopigwa marufuku Februari 2015, wakisingizia majibu yamekuwa hivyo baada ya kula nyama ya nguruwe mwitu. Mkulima amesema aliahidiwa kupewa £25,000 ili aseme ameiuzia nyama Timu Furry, lakini promota Frank Warren ameyaita madai hayo ni uzushi mtupu. Akipatikana na hatia ya kuvuruga uchunguzi wa kwanza, ambao unafuatia na vipimo vilivyoonyesha kuwa ametumia dawa hizo, anaweza kufungiwa kwa miaka minane. Martin Carefoot alitoa ushahidi kwenye uchunguzi akisema aliipa timu nyama ya nguruwe mwitu, lakini alipohojiwa kwenye gazeti alisema hajafanya hivyo. Gazeti la Mail jana liliripoti kuwa mkulima huyo amesema aliombwa asaidie na rafiki yake ambaye anaifahamu Timu Fury, lakini hakupewa malipo aliyoahidiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako