• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi 20 za Afrika kusini mwa Sahara zaripoti maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-16 09:56:52

    Hadi kufikia jana nchi zisizopungua 20 za Afrika kusini mwa Sahara zimeripoti visa vya maambukizi ya COVID-19, Afrika Kusini ikiwa imeripoti watu 38 walioambukizwa virusi hivyo. Nchi mbalimbali zimechukua hatua za kinga na udhibiti wa ugonjwa huo.

    Uganda imeimarisha hatua za kinga na udhibiti baada ya nchi jirani za Kenya, Rwanda na DRC kuwa na watu wenye maambukizi.

    Wizara ya Afya ya Uganda imetoa namba ya simu ya kuripoti mtu yeyote anayeshukiwa kuambukizwa COVID-19 na kusambaza habari kuhusu ugonjwa huo.

    Nchi hiyo tayari imepokea vifaa vyenye thamani ya karibu dola 55,000 za Kimarekani kusaidia kuzuia kuenea kwa virusi. Hatua za ukaguzi na upimaji zimetekelezwa katika vivuko vyote vya kuingilia nchini, zikiwa ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe, vivuko vya Malaba na Busia kwenye mpaka na Kenya, Cyanika kwenye mpaka na Rwanda, na Elegu kwenye mpaka na Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako