• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaandaa sera za nguvu zaidi kufufua uchumi ulioathiriwa na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-16 16:55:17

    China inajiandaa kuchukua sera za nguzu zaidi ili kufufua uchumi wake na kutuliza upatikanaji wa ajira wakati takwimu za hivi karibuni kuhusu uzalishaji viwandani, mauzo ya rejareja na uwekezaji zikionyesha kushuka katika miezi miwili ya mwanzo ya mwaka huu kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19.

    Mamlaka ya Takwimu ya Taifa ya China (NBS) imesema uzalishaji viwandani, ambao ni kiashiria muhimu cha uchumi, ulishuka kwa asilimia 13.5 ikilinganishwa na mwaka jana katika kipindi cha mwezi Januaru hadi Februari. Uwekezaji wa mali zisizohamishika ulishuka kwa asilimia 24.5, huku mauzo ya nyumba na bidhaa za mahitaji ya kila siku ikishuka kwa asilimia 20.5.

    Ili kukabiliana na mshtuko wa kiuchumi kutokana na janga hilo, mamlaka za kifedha nchini China zimeahidi kufuatilia zaidi sera nyumbufu ili kuwa na fedha za kutosha na kufanya mageuzi ya kiwango cha riba ya malipo ya mkopo.

    Mamlaka hiyo inatabiri kuwa kutokana na kuongezeka kwa kasi ya biashara na hali kuanza kurejea kuwa ya kawaida, sekta ya uchumi itaanza kuonyesha kufufuka mwezi huu na robo ya pili ya mwaka kutokana na kupungua kwa athari za maambukizi ya virusi vya korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako