• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jukwaa lililoanzishwa na CMG latoa ajira laki moja 

    (GMT+08:00) 2020-03-16 16:59:59

    Jukwaa la ajira mtandaoni lililoanzishwa tarehe 2 mwezi huu na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG kwa kushirikiana na Kamati ya Mali za Kitaifa ya Baraza la Serikali la China limetoa ajira zaidi ya laki moja kwa jamii.

    Madhumuni ya kuanzishwa kwa jukwaa hilo ni kutatua tatizo la upungufu wa wafanyakazi wa makampuni yanayopanga kurejesha uzalishaji, huku baadhi ya watu wakikosa njia za kutafuta kazi kutokana na maambukizi ya COVID-19.

    Takwimu mpya zinaonesha kuwa, hadi sasa jukwaa hilo limevutia makampuni 2,500, na idadi hiyo inaendelea kuongezeka. Kwa upande mwingine, tovuti ya jukwaa hilo imesomwa na watu zaidi ya milioni 10, na kati yao laki tatu wametoa maombi ya kutafuta kazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako