• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi mbalimbali zaongeza nguvu kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-16 17:21:21

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema, mpaka kufikia jana saa 10 kwa saa za Ulaya ya kati, nchi 143 licha ya China, zina kesi elfu 72,469 za maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19, na nchi hizo zimetoa hatua kali zaidi kukabiliana na mlipuko wa virusi hivyo.

    Meya wa mji wa New York Bw. Bill de Blasio ametoa wito kwa serikali ya Marekani kuendelea kuruhusu upimaji wa moja kwa moja wa maambukizi ya virusi hivyo, kutumia jeshi kukarabati majengo husika kama hospitali maalum, na pia ametangaza kufungwa kwa shule zote katika mji huo kuanzia leo.

    Ufaransa pia imetangaza kuingia kwenye kipindi cha ngazi ya juu zaidi ya kupambana na virusi hivyo. Mamlaka nchini humo zimeamuru kufungwa kwa maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu ikiwemo migahawa, baa, na majumba ya sinema.

    Ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya korona, Ujerumani imefunga mpaka wake na Ufaransa, Austria na Uswizi.

    Rais wa Korea Kusini Bw. Moon Jae-in ametangaza kuwa, katika siku zijazo, serikali yake itatoa asilimia 50 ya fedha zinazotumiwa kufufua maeneo ya mji wa Daegu na Gyeongsangbuk-Do.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako