• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yahisiwa kuwa chanzo cha COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-16 19:21:59

    Hivi karibuni, Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa cha Marekani Robert Redfield alisema kwenye mkutano wa baraza la wawakilishi la bunge la nchi hiyo kuhusu ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19, kuwa baadhi ya watu waliodhaniwa kufariki kwa mafua huenda walifariki kutokana na virusi hivyo. Kauli hii ni sawa na kukiri makosa iliyofanya Marekani katika kugundua vifo vilivyotokana na virusi vya korona, na pia ni sababu ya kuitilia mashaka Marekani kuwa ni chimbuko la virusi vipya vya korona.

    Msimu wa mafua nchini Marekani ulianzia mwezi Septemba mwaka jana, na mwezi Oktoba, wachezaji wa jeshi la Marekani walikwenda Wuhan kushiriki kwenye mashindano ya saba ya Majeshi Duniani, na kuna wachezaji wa kigeni waligunduliwa kuwa na magonjwa ya kuambukizwa kabla ya kufika mjini humo. Mwezi Disemba mgonjwa wa kwanza wa virusi vya korona aligunduliwa mjini Wuhan. Marekani imekiri baadhi ya vifo vilivyodhaniwa kutokana na ugonjwa wa mafua, vilitokana na virusi vya korona, hivyo kuna mantiki kwa watu kutia shaka kuwa virusi vya korona vilianzia Marekani.

    Hivi karibuni, kundi la washauri wabingwa nchini Canada Global Research limetoa makala katika tovuti yake likisema, kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na wataalam wa virusi wa kisiwani Taiwan juu ya chanzo cha virusi nchini Iran na Italia, mpangilio wa vinasaba vya virusi katika nchi hizo mbili ni tofauti na ule wa China, na hii inamaanisha kuwa havitokei China.

    Wanasayansi wamefanya tafiti mbalimbali. Tarehe 24, Januari gazeti la The Lancet la Marekani toleo la mtandao wa internet lilichapisha tasnifu ya utafiti iliyoandikwa na madaktari saba wa hopitali ya Jinyintan mjini Wuhan. Madaktari hao waliwafanyia utafiti wagonjwa 41 wa mwanzo waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya korona, na waligundua kuwa 13 kati yao hawakufika katika soko la vyakula vya bahari la Huanan. Tarehe 26, Januari, jarida la the Science lilitoa makala yenye kichwa cha "soko la vyakula vya bahari la Huanan mjini Wuhan huenda sio chimbuko la virusi vipya vya korona", likinukuu maoni ya mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza wa Chuo Kikuu cha Georgetown nchini Marekani Daniel Lucey akisema watu hao 13 hawana uhusiano na soko hilo, na kama ni hivyo, huenda virusi vipya vya korona vilianzia sehemu nyingine.

    Hivi sasa kazi za kuzuia maambukizi ya virusi vya korona duniani ziko katika kipindi muhimu. Hadi tarehe 15, Machi, kesi 72,469 za virusi vya korona zilikuwa zimeripotiwa nje ya China, huku idadi ya vifo ikifikia 2,531, nchi nyingi ikiwemo Marekani zimetangaza hali ya dharura. Hivyo huu ni wakati muhimu kwa Marekani kueleza virusi vya korona vilianza lini na wapi kwa mujibu wa sayansi, jambo ambalo sio tu ni la kuwajibika kwa maisha na afya ya watu wa Marekani, bali pia ni kitendo cha lazima cha kuzuia maambukizi ya virusi na kulinda afya ya umma duniani.

    Hivi sasa, wanasayansi wa nchi mbalinbali wanajitahidi kutafuta chimbuko la virusi, na jumuiya ya kimataifa pia ina maoni tofauti na hili. Lakini mashaka na wasiwasi unatakiwa kutokana na sayansi na ukweli, wala sio upotoshaji na kufanya mashambulizi. Mbali na kufanya vizuri kazi za kuzuia maambukizi ya virusi vya korona, Marekani inatakiwa kutoa ushirikiano na nchi nyingine kwa sayansi, taaluma na kuwajibika, na kutafuta jibu la chimbuko la virusi, kujibu wasiwasi na umma kwa uhalisia na kutoa maelezo sahihi kwa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako