• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Cristiano Ronaldo kupewa mkataba wa miaka minne Juventus

  (GMT+08:00) 2020-03-17 08:22:06

  Juventus Kibibi 'Kizee cha Turin' imepanga kumpa mkataba mpya Cristiano Ronaldo utakaomalizika mwaka 2024. Mkataba huo utamfanya Ronaldo kusherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa na miaka 39 ndani ya klabu hiyo. Juventus inataka kumbakiza nyota huyo aliyefunga mabao 42 katika mechi 53 tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Real Madrid mwaka 2018. Licha ya kubakiza miaka miwili kabla ya mkataba kumalizika, klabu hiyo inataka kumpiga kitanzi nahodha huyo wa Ureno kutokana na mafanikio aliyopata. Ronaldo anayelipwa mshahara wa Pauni500,000 kwa wiki katika mkataba wake wa miaka minne, amekuwa kinara wa mabao Juventus. Juventus inataka huduma ya Ronaldo aliyetimiza miaka 35 Februari, ili baadaye awaongoze washambuliaji wapya ambao watasajiliwa na klabu hiyo. Harry Kane, Gabriel Jesus, Mauro Icardi na Timo Werner wako katika mawindo ya Juventus. Ronaldo ametimkia nyumbani kwao Madeira muda mfupi baada ya Italia kukumbwa na maambukizi ya virusi vya korona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako