• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KORONA: Patrick Cutrone agundulika na virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-03-17 08:23:10

    Patrick Cutrone mshambuliaji wa Fiorentina aliyetua hapo kwa mkopo akitokea Wolves amegundulika na virusi vya korona na kufanya idadi ya waathirika kufikia wanne ndani ya klabu hiyo ya Italia. Nyota huyo wa Wolves anakipiga kwa mkopo kwenye Klabu ya Fiorentina inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia ya Serie A. Nyota huyo alijiunga na klabu hiyo kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari kwa mkataba wa miezi 18 na atadumu mpaka mwaka 2021. Mchezaji mwingine ndani ya Fiorentina ambaye ameathirika na Corona ni German Pezzella baada ya kufanyiwa vipimo. Taarifa rasmi kutoka ndani ya Klabu ya Fiorentina imeeleza kuwa wachezaji wake Patrick Cutrone na German Pezzella na mtaalamu wa masuala ya afya Stefano Dainelli wana korona ila kwa sasa wanaendelea vizuri pamoja na mshambuliaji Dusan Vlahovic. Naye kocha mkuu wa klabu ya Flamengo ya nchini Brazil Jorge Jesus ,65, jana usiku alithibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya COVID19 vinavyoleta homa kali ya mapafu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako