• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping asema China itatuma wataalamu zaidi wa matibabu nchini Italia

  (GMT+08:00) 2020-03-17 09:29:03

  Rais Xi Jinping wa China amesema, China itatuma wataalamu zaidi wa matibabu nchini Italia, pia itafanya juhudi kadiri iwezekanavyo kutoa vifaa vya matibabu na misaada mingine kwa Italia.

  Akiongea jana kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Italia Bw. Giuseppe Conte, Rais Xi amesema serikali ya Italia imechukua hatua mfululizo za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19. Amesema China inaiunga mkono Italia, na pia ina imani kuwa Italia itapata ushindi dhidi ya virusi hivyo.

  Bw. Conte ameishukuru China kwa msaada wake, na pia ameeleza imani kuwa urafiki kati ya nchi hizo mbili utaimarishwa zaidi baada ya mapambano dhidi ya COVID-19.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako