• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema idadi ya wagonjwa wa COVID-19 duniani inakaribia laki 1.7

    (GMT+08:00) 2020-03-17 09:39:12

    Shirika la afya duniani WHO limetoa ripoti ya kawaida ikisema, hadi kufikia jana asubuhi, nchi na kanda 152 zimeripoti watu 167,511 waliothibitishwa kuambukizwa COVID-19, idadi ambayo imeongezeka kwa watu 13,903 ikilinganishwa na siku iliyotangulia.

    Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya jumla ya vifo vilivyotokana na ugonjwa huo duniani imeongezeka kwa watu 862 na kufikia 6,606 katika saa 24 zilizopita.

    Nje ya China, maambukizi 13,874 mapya yameripotiwa na kusababisha idadi ya wagonjwa kufikia 86,434, huku wagonjwa 3,388 wakifariki.

    Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw. Tedros Ghebreyesus amesema, wagonjwa na vifo vingi zaidi kutokana na COVID-19 hivi sasa vimeripotiwa nje ya China, huku akisisitiza umuhimu wa kufanya upimaji na kuwaweka wagonjwa kwenye karantini ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako