• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Safaricom yashirikiana na serikali kusambaza habari kuhusu COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-17 09:39:43

    Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imesema inashirikiana na serikali kuongeza ufahamu wa umma kuhusu visa vinavyoshukiwa kuwa vya ugonjwa wa COVID-19 nchini humo.

    Kampuni hiyo imesema kituo cha mawasiliano ya simu na namba maalum ya simu, kimezinduliwa na kamati ya mwitikio wa dharura wa taifa kuhusu COVID-19, ili kuwafahamisha wakenya jinsi ya kujikinga na kudhibiti virusi hivyo.

    Mkurugenzi mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Bw. Michael Joseph ametoa taarifa ikisema, wameunganisha mitandao mingine kuhakikisha kwamba wateja wao wanaweza kupiga simu kwenye kituo cha simu. Simu zote zinazopigiwa kwenye namba 719 ni bure. Na wanafanya juhudi kushirikiana na pande zote kusaidia kukabiliana na msukosuko huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako