• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yasimamisha mikusanyiko ya kijamii kutokana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-17 10:09:42

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ametangaza kusimamishwa kwa mikusanyiko yote ya kijamii kama michezo, shughuli za kidini, kiutamaduni na kisiasa kutokana na tishio la COVID-19.

    Rais Kiir amesema ingawa nchi hiyo bado haijakumbwa na virusi vya Korona, umma unatakiwa kuwa na tahadhari sahihi za kujikinga ili kuepuka kuambukizwa ugonjwa huo, akiongeza kuwa mikutano yote ya kimataifa itakayofanyika mjini Juba imesimamishwa kwa muda kwa sababu ya tishio la COVID-19, na kuweka tahadhari zaidi mahali pa kazi.

    Aidha maafisa wanne wa serikali waliokwenda nchi zenye maambukizi ya COVID-19 wamewekwa kwenye karantini, na naibu waziri wa afya wa nchi hiyo Bw. Makur Matur Kariom amesema hatua hiyo ni kwa ajili ya kusaidia kuchukua tahadhari kulinda nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako