• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kiwango cha kurejea kwa uzalishaji nchini China chafikia asilimia 90 isipokuwa mikoa michache

  (GMT+08:00) 2020-03-17 17:47:15

  Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China imesema kiwango cha kurejea kwa uzalishaji nchini humo kimefikia zaidi ya asilimia 90 isipokuwa mikoa michache ukiwemo Hubei, na shughuli za uzalishaji za kampuni za nje pia zinarudi katika hali ya kawaida.

  Msemaji wa Kamati hiyo Meng Wei leo hapa Beijing amesema, hivi sasa viwanda vikubwa hapa China viko mbioni kurejesha uzalishaji, na kiwango cha kurejea kwa uzalishaji katika baadhi ya mikoa na miji ikiwemo Shanghai kimefikia karibu asilimia 100. Anasema,

  "Kwa mujibu wa hali ya matumizi ya umeme iliyosimamiwa na shirika la umeme, hivi sasa matumizi hayo katika kampuni zinazojikita katika sekta ya medali zisizo za chuma yamerejea katika kiwango cha kawaida cha mwaka jana, na matumizi ya umeme katika sekta za matibabu, kemikali na elektroniki yamerejea kwenye asilimia zaidi ya 90 ya kiwango cha kawaida, na matumizi ya umeme katika sekta za chuma, mashine na nguo yamerejea kwenye asilimia zaidi ya 80 ya kaiwada, na sekta za usafiri wa anga, bandarini na uchukuzi baharini zinafanya shughuli zao kama kawaida."

  Baada ya kutokea kwa maambukizi ya virusi vipya vya korona, kampuni za ndani na nje ya China zilikumbwa na changamoto kutokana na vizuizi vya usafirishaji wa watu na vitu, wafanyakazi kushindwa kufika kazini kwa sababu ya kuwekwa karantini na ukosefu wa vifaa vya kujikinga na virusi. Juu ya hilo, naibu mkuu wa idara ya mitaji ya kigeni ya Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Wu Hongliang amesema, kutokana na kupungua kwa maambukizi ya virusi vya korona na kuongezeka kwa kiwango cha kurejea kwa shughuli za uzalishaji hapa China, oda zinazopokelewa na kampuni za kigeni zilizopo China zinaongezeka, jambo linaloongeza imani za kampuni hizo kuharakisha kurejesha uzalishaji wao.

  Wu pia amesisitiza kuwa licha ya kutokea kwa maambukizi hayo, sifa nzuri ya mnyororo wa uzalishaji nchini China haijabadilika.

  "China ina soko kubwa la ndani, na masoko katika sekta nyingi kama vile magari na vifaa vya teknolojia ya juu ni makubwa zaidi duniani. Wakati huohuo, China ina utaratibu mkubwa na wa aina nyingi wa uzalishaji viwandani, ambao unajumuisha mnyororo mzima kutoka utafiti hadi utengenezaji. Katika mchakato wa uzalishaji, bidhaa zinaboreshwa mara kwa mara, jambo ambalo ni muhimu kwa sekta nyingi."

  Hivi karibuni, Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China ilitangaza hatua 11 za kutuliza uwekezaji wa kigeni. Wu amesema hatua hizo zitazisaidia kampuni za nje kutatua changamoto zinazozikabili katika kurejesha shughuli za uzalishaji, kupanua maeneo yanayoruhusiwa kuwekezwa na mitaji ya kigeni, na pia kuongeza nguvu ya kuharakisha utekelezaji wa miradi iliyowekezwa na mitaji ya kigeni. Wu amesema China kuendelea kufungua mlango kwa nje kutasaidia kuongeza imani ya kampuni za kigeni ya kufanya shughuli zao nchini China na kuchangia utulivu wa mnyororo wa uzalishaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako