• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahudumu wa afya waliokwenda Hubei kusaidia kupambana na COVID-19 warejea makwao

    (GMT+08:00) 2020-03-17 19:33:22

    Msafara wa gari lililobeba wahudumu wa afya 43 wa kikundi cha matibabu cha dharura cha mkoa wa Shaanxi leo asubuhi ulifunga safari ya kurejea mkoani humo, ikiwa ni kikundi cha kwanza cha madaktari kuondoka mkoani Hubei baada ya kuusaidia mkoa huo katika mapambano dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.

    Jana, Kamati ya Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ilifanya mkutano na kuamua kuwa, vikundi vya madaktari vilivyousaidia mkoa wa Hubei vitaondoka hatua kwa hatua. Kutokana na mpango huo, leo, watu 3,675 wa vikundi 41 vya madaktari wameanza safari ya kurejea makwao. Vikundi hivyo vilisaidia hospitali 14 za muda na hospitali 7 zilizochaguliwa kuwapokea wagonjwa wa COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako