• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kwa nini hatua za Marekani kukabiliana na COVID-19 zinakosolewa

    (GMT+08:00) 2020-03-17 20:15:49

    Soko la hisa la Marekani jana liliporomoka tena, na vigezo vya Dow vilishuka kwa asilimia 13, kiasi hicho ni kikubwa zaidi katika miaka zaidi ya 30 iliyopita. Rais Donald Trump wa nchi hiyo kwa mara ya kwanza amekiri kuwa uchumi wa Marekani unaelekea kudidimia kutokana na ugonjwa wa COVID-19. Lakini alipotathmini hatua alizochukua kukabiliana na ugonjwa huo, alisema ni alama 10.

    Hata hivyo, hatua hatua hizo zimekosolewa vikali na Wamarekani na vyombo vya habari vya nchi hiyo, wakisema serikali yao imeruhusu maambukizi ya virusi kuenea, viongozi wake hawakufanya vizuri, na kuchelewa kuchukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huo.

    Badala ya kujikosoa, rais Tump amepaka matope China kwa kusema virusi vipya vya korona ni virusi vya kichina. Kabla ya hapo, mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa nchini Marekani (CDC) Robert Redfield alikiri kuwa, mafua yaliyoanza mwezi Septemba mwaka jana yamesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 20, na ukweli ni kwamba baadhi ya wagonjwa waliodhiniwa kuambukizwa mafua walikuwa wameambukizwa virusi vipya vya korona.

    Kauli ya Trump imelaumiwa na watu wa hali mbalimbali. Daktari mmoja wa Marekani Eugene Gu amesema ana wasiwasi mkubwa baada ya kusikia Trump kuita virusi vya korona kuwa virusi vya Kichina.

    Hivi sasa Wamarekani wanafuatilia sana mchakato wa taratibu wa upimaji virusi nchini humo, kwani hali hii imesababisha watu wengi kuchelewa kupimwa. Watu wanalalamika kuwa serikali ya nchi hiyo haikutilia maanani ugonjwa huo, na CDC haifanyi kazi vizuri.

    Aidha, habari za kupotosha zilizotolewa na serikali ya Marekani pia zimekosolewa na watu wengi. Gazeti la Washington Post limesema ndani ya mwezi mmoja, serikali ya Trump imetoa habari zinazogongana kwa mara 14.

    Twitter ni mtandao wa kijamii unaotumiwa zaidi na Wamarekani. Kwenye mtandao huo, watu wamelalamikia sana hatua zilizochukuliwa na serikali ya Marekani katika kupambana na COVID-19. Kwa mfano, tarehe 28 mwezi Februari kwenye Twitter CDC ilisema haipendekezi watu kutumia mask kukinga virusi. Tamko hilo limelaniwa vikali na watu wengi, wakisema CDC ni "mdanganyifu".

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniai Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, hatua madhubuti zilizochukuliwa na China zilitoa nafasi kwa dunia kujiandaa na mlipuko wa COVID-19. Lakini serikali ya Marekani haijatumia fursa hiyo. Labda ukweli ni kwamba, ugonjwa huo umeenea nchini Marekani mapema kuliko nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako