• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KORONA: UEFA yatangaza kuahirisha michuano ya mataifa Ulaya (Euro 2020)

    (GMT+08:00) 2020-03-18 08:22:24

    Shirikisho la soka Ulaya (UEFA) mapema jana lilitangaza kuahirishwa kwa michuano ya mataifa Ulaya (Euro 2020) yaliyokuwa yafanyike kipindi cha majira ya joto mwaka huu. UEFA wametangaza kuahirisha michuano hiyo hadi mwaka 2021 sasa itakuwa ni Euro 2021 sio 2020 tena, hata hivyo UEFA pia inapanga kumaliza michuano yote ya vilabu Ulaya June 30 endapo maambukizi ya korona yatazidi. Kutokana na kuenea kwa Virusi vya Corona ambavyo vilianza kusambaa mwezi Januari, wamesitisha michuano hiyo na inatarajiwa kuanza kufanyika 2021 kati ya Juni 11 mpaka Julai 11 mwaka ujao. Mechi zote za UEFA na mechi za kirafiki kwa klabu na timu za Taifa kwa Wanawake na Wanaume zinasitishwa mpaka pale itakapotolewa taarifa, mechi zilizotarajiwa kuchezwa mwezi Machi sasa zinaweza kuanza mwezi Juni lakini itategemea na hali itakavyokuwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako