• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • GOFU: Mashindano ya Diplomatic Golf kuunguruma Mei 30, 2020

  (GMT+08:00) 2020-03-18 08:22:53

  Mashindano ya Diplomatic Golf msimu wa pili yanayoratibiwa na Kampuni ya Tanzania Mwandi kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, yanatarajiwa kuanza kuunguruma Mei 30, 2020 katika viwanja vya Kilimanjaro Golf Club, Usa River jijini Arusha. Maandalizi ya mashindano hayo ambayo yanafanyika kila mwaka, yameendelea kwa nguvu jana Jumanne, Machi 17, 2020, katika Viwanja Gymkhana jijini Dar es Salaam. Akizungumza viwanjani hapo wakati wa maandalizi hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, amesema maadalizi hayo yanaendelea vizuri na kwa kiwango cha juu. Diplomatic Golf, ni fursa mahsusi kwa mawaziri, wabunge, wanasiasa, wanadiplomasia na wananchi wote wa kawaida kukutana na kubadilishana uzoefu wa mchezo huo na kutengeneza njia mbadala ya kuikuza tasnia hiyo kwa kushirikiana na wadau na wapenda golf. Mwaka 2019, Mashindano ya Diplomatic Golf yalifanyika visiwani Zanzibar katika Viwanja vya Zanzibar Golf Course Sea Cliff, ambapo mwaka huu yanatarajiwa kuwa tofauti huku vitu vingi vikiwa vimeboreshwa zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako