• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nusu ya wagonjwa wa COVID-19 watoka hospitali ya Leishenshan ya Wuhan baada ya kupona

  (GMT+08:00) 2020-03-18 09:26:35

  Naibu mkurugenzi wa hospitali ya Leishenshan ya Wuhan Bw. Yuan Yufeng jana kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, karibu nusu ya wagonjwa wa COVID-19 waliopewa matibabu kwenye hospitali hiyo wameruhusiwa kutoka baada ya kupona.

  Bw. Yuan amesema, hadi kufikia Jumatatu, hospitali ya Leishenshan ilikuwa imepokea wagonjwa 1,961 wa COVID-19 na wagonjwa 970 kati yao wametoka. Bw. Yuan ameongeza kuwa, hospitali hiyo ina wafanyakazi wa matibabu 3,202 wa timu 16 za matibabu kutoka mikoa tisa, pamoja na wahudumu 660.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako