• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • WHO yatoa wito kwa nchi za Ulaya kujifunza uzoefu wa China katika kupambana na COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-03-18 10:01:44

  Mkuu wa Shirika la afya duniani (WHO) barani Ulaya Bw. Hans Kluge ametoa wito kwa nchi za Ulaya kuchukua hatua za kijasiri zaidi za kuzuia nimonia ya COVID-19, na kusisitiza haja ya kuwahamasisha na kuwashirikisha watu wote katika kuzuia na kudhibiti janga hilo.

  Bw. Kluge amesema hayo baada ya kufanya mkutano kwa njia ya simu na maafisa wa afya kutoka nchi 53 za Ulaya, akiongeza kuwa karibu watu laki 1.8 duniani wameambukizwa virusi hivyo, theluthi moja kati yao wako barani Ulaya na kuifanya Ulaya kuwa kiini cha mlipuko wa COVID-19. Bw. Kruger ameongeza kuwa ingawa janga hilo limeenea katika nchi zaidi ya 150, China, Korea Kusini, Singapore na nchi nyingine zimepata mafanikio halisi katika kudhibiti virusi hivyo, na uzoefu wa China unaonyesha kuwa kuwatambua na kuwafuatilia watu waliokaribiana na wagonjwa kwa haraka, na kuchukua hatua za kutenganisha watu, kuna ufanisi wa kuzuia maambukizi na kuokoa maisha ya watu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako