• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya kuweka vizuizi vya kusafiri ili kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-18 10:02:05

    Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wamefanya mkutano wa kilele kwa njia ya video na kukubali kupitisha hatua kadhaa ikiwemo kuweka vizuizi vya kuingia kwa watu kutoka nje ya Umoja wa Ulaya ili kukabiliana na janga la nimonia ya COVID-19.

    Mkutano huo umeamua kuridhia pendekezo la Tume ya Ulaya kuweka vizuizi vya kuingia kwa watu kutoka nje wa Umoja wa Ulaya kwa kipindi cha awali cha siku 30, wakati huo huo Umoja huo utahakikisha ugavi na usafirishaji wa dawa, chakula na bidhaa, na raia wa umoja huo wanaweza kurudi katika nchi zao.

    Mkutano huo pia umeamua kukubali hatua zilizopendekezwa na Tume ya Ulaya kuzuia kuuza vifaa vya matibabu kwa nje, na kampuni ikitaka kuuza nje vifaa vya matibabu, kama vile mask, kwa kanda nyingine lazima ipate idhini ya serikali ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako