• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yasitisha utoaji viza kwa raia wa nchi kadhaa zilizoathiriwa na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-18 10:35:21

    Mawaziri wa Afrika Kusini jana wamefanya mkutano na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Johannesburg, na kueleza maendeleo ya kazi ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya COVID-19.

    Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Aaron Motsoaledi amethibitisha kuwa baada ya Afrika Kusini kutangaza hali ya janga la taifa, serikali imeamua kusitisha utoaji wa viza na kufuta viza zilizotolewa miezi miwili iliyopita mwaka huu kwa raia wa Italia, Marekani, China na Iran.

    Bw. Motsoaledi pia amesema, vivuko vya mpakani kati ya Afrika Kusini na Zimbabwe, na kati yake na Swaziland havitafungwa kutokana na COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako