• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Sadio Mane atoa msaada wa KSh 5 milioni kwa taifa lake kukabiliana na coronavirus

  (GMT+08:00) 2020-03-18 16:20:48

  Sadio Mane ameendelea kuwa mwaminifu kwa taifa lake Senegal licha ya kujipatia utajiri wake barani Ulaya. Mshambuliaji huyo wa Liverpool kwa mara nyingine tena amethibitisha ukarimu wake baada ya kuripotiwa kutoa mchango wa pauni 45,000 kusaidia kudhibiti virusi vya corona nchini Senegal. Winga huyo pia aliwaomba maafisa wa afya katika taifa lake kuwa makini. Si mara ya kwanza kwa Mane kuwa mkarimu kwa watu wake, mzawa huyo wa Senegal pia amejenga hospitali na shule kusaidia kijiji chake kuwa na maendeleo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako