• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chanjo za COVID-19 zinazotengenezwa na China kuingia kwenye kipindi cha majaribio kwa watu hivi karibuni

    (GMT+08:00) 2020-03-18 18:03:49

    Baadhi ya chanjo za virusi vipya vya korona zinazotengenezwa nchini China zinatarajiwa kuingia kwenye kipindi cha majaribio kwa watu hivi karibuni.

    Msomi kutoka Chuo cha Ufundi cha China, Wang Junzhi amesema, wanasayansi wa China wamefanya juhudi kuendeleza chanjo ya virusi hivyo kwa kutumia njia tano, na kwamba usalama wa chanjo umepewa kipaumbele kikubwa katika utafiti na kuendeleza chanjo hizo. amesema utafiti na maendeleo ya chanjo hizo nchini China, ambao unaendana na ule wa wanasayansi wa nchi za nje, umefanyika kwa njia ya kisayansi, katika ubora na kwa utaratibu.

    Ofisa kutoka Wizara ya Elimu ya China Lei Chaozi amesema, chanjo inayotokana na msingi wa virusi vya mafua kwa sasa inafanyiwa majaribio kwa wanyama ili kuhakikisha usalama na ufanisi wake, na imepangwa kufanyiwa majaribio kwa binadamu mwishoni mwa mwezi ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako