• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaharakisha kuanza tena utekelezaji wa miradi mikubwa

    (GMT+08:00) 2020-03-18 18:12:02

    Baraza la Serikali La China limesema litaharakisha kuanza tena utekelezaji wa miradi mikubwa ya uwekezaji ili kuwanufaisha wananchi, pia limesisitiza kuhimiza kuharakisha miradi mikubwa elfu 11 inayoendelea nchini kote.

    Katika mkutano wake uliofanyika jana, Baraza hilo limesisitiza kuwa kazi ya kuanza tena utekelezaji wa miradi mikubwa ya uwekezaji lazima ipewe kipaumbele kwenye kazi za kutuliza uwekezaji na kuongeza mahitaji ya ndani. Pia inahitaji kutatua masuala yanahusika na miradi hiyo, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi, utoaji wa malighafi, fedha, na vifaa vya kujikinga na virusi, ili kuharakisha mchakato wa ujenzi wa miradi mikubwa inayoendelea nchini kote. Mbali na hayo, pia maandalizi mazuri yanapaswa kufanyika kwa miradi mipya zaidi ya elfu nne iliyopangwa kuanzishwa mwaka huu, na kusaidia kuidhinisha miradi mikubwa ili kazi ya ujenzi wa miradi hiyo ianze haraka iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako