• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda kupata dola milioni 85.9 kutoa EU

    (GMT+08:00) 2020-03-18 19:03:10
    Uganda imesaini makubaliano ya nyongeza ya fedha za ruzuku yenye thamani ya dola milioni 85.9 kutoka kwa Jumuiya ya Ulaya.

    Waziri wa Fedha Matia Kasaija alisema misaada ya EU itasaidia miradi na programu tatu ambazo zinalenga kuboresha viwango vya bidhaa za Uganda, na kuwezesha nchi kupata vibali na kuendela kuuza bidhaa zake kwenye soko la Ulaya.

    Bwana Kasaija alisema idadi kubwa ya fedha hizo karibu dola milioni 50 zitafadhili mpango wa uchumi usiochafua mazingira, ambao unajumuisha kukuza bidhaa na miradi ambayo hupunguza hatari za mazingira.

    Balozi wa Umoja wa Ulaya Attilio Pacifici ambaye alisaini kwa niaba ya umoja huo alisema programu ya kuongeza uzalishaji uziochafua mazingira ni kama vile miji safi, kawi endelevu na matumizi ya gesi nyumbani na viwandani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako