• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima kupata elimu ya kilimo

    (GMT+08:00) 2020-03-18 19:06:05

    Zaidi ya teknolojia 30 za mazao mbalimbali ya kilimo, zinatarajiwa kuonyeshwa na Kituo cha Utafiti wa Mazao ya Kilimo (Tari) mjini Mbeya kwa lengo la kutoa elimu kwa wakulima na kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya nafaka na mboga.

    Mkurugenzi wa Kituo hicho, Dk. Tulole Bucheyeki, alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonyesho hayo ambayo alisema yamefikia asilimia 85.

    Dk. Bucheyeki alisema maonyesho hayo yanalenga kuwasaidia wakulima kuwapa mbinu na teknolojia za kisasa kwenye kilimo cha mazao ya nafaka na mboga.

    Alisema teknolojia 30 ambazo walibuni zitaleta tija kwa wakulima kwa kuwa kupitia mashamba darasa yao yamekuwa kivutio kwa wengi wakihitaji kufundishwa.

    Alisema maonyesho ya teknolojia hiyo ambayo yanalenga kwenye kilimo biashara, yalianza tangu Desemba 20 mwaka 2019 na yanatarajiwa kumalizika Mei 9, mwaka huu na imani yake kila mkulima atakayetembelea maonyesho hayo ambayo yanafanyika katika ofisi za kituo hicho watazalisha kwa tija na kuongeza mavuno.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako