• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaihimiza Marekani iache kukandamiza vyombo vya habari vya China

    (GMT+08:00) 2020-03-19 08:48:01

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang jana Jumatano amesisitiza kuwa hatua zilizochukuliwa na China ni jibu la lazima kwa vitendo vya Marekani vya kukandamiza ofisi za vyombo vya habari vya China nchini humo. Amesema China inaitaka Marekani iache vitendo hivyo mara moja, la sivyo Marekani itapata hasara kubwa zaidi.

    Kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika jana, Bw. Geng Shuang amesema ofisi za vyombo vya habari vya China nchini Marekani siku zote zinafuata sheria za Marekani na kufuata maadili ya kazi. Marekani haitakiwi kuhukumu vyombo vya habari vya nchi nyingine kwa vigezo vyake kutokana na upendeleo wa kiitikadi, na pia haitakiwi kuchukua hatua za kibaguzi na kikandamizi dhidi ya vyombo vya habari vya China bila msingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako