• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria yatangaza kufuta viza zilizotolewa kwa watu kutoka nchi zinazokumbwa na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-19 08:55:53

    Ikiwa hatua ya kupambana na mlipuko wa COVID-19, serikali ya Nigeria jana imetangaza kufuta viza zilizotolewa kwa watalii kutoka nchi 13 zinazokumbwa na virusi hivyo.

    Nchi hizo ni pamoja na China, Italia, Iran, Korea Kusini, Hispania, Japan, Ufaransa, Ujerumani, Norway, Marekani, Uingereza, Uholanzi, na Uswisi.

    Waziri wa mambo ya ndani wa Nigeria Rauf Aregbesola amesema, nchi hizo zote zina maambukizi zaidi ya 1,000 ya virusi hivyo, na Nigeria imesitisha utoaji wa viza na itafuta viza zilizotolewa kwa watalii kutoka nchi hizo. Vilevile amesema hatua hiyo itatekelezwa kwa muda wa wiki nne kuanzia Jumamosi, na hatua zijazo zitategemea maendeleo ya hali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako