• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Lionel Messi avurugana tena na uongozi wa klabu yake Barcelona

  (GMT+08:00) 2020-03-19 08:56:32

  Kwa mara ya pili mwanasoka nyota Lionel Messi wa Barcelona amevurugana na uongozi wa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uhispania LaLiga. Raia huyo wa Argentina ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, alianza kukwaruzana na Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo, Eric Abidal aliyeshutumu wachezaji kwa kutojitolea na kusababisha kutimuliwa kwa kocha Ernesto Valverde. Akimjibu, Messi alimwita bosi huyo muongo mkubwa kwa kuwa alishindwa kutaja majina ya wale waliokuwa wazembe kikosini. Lakini mara hii, ni Messi aliyeamsha vurugu akidai kwamba hana mpango wa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuchezea klabu hiyo ya Catalunya. Messi amesema ameamua kuondoka baada ya wakuu wa klabu hiyo kushindwa kukamilisha usajili wa rafiki yake wa dhati Neymar Junior anayechezea klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) nchini Ufaransa. Kutokana na kuchelewa huko, Messi amewaambia wazi viongozi wa klabu hiyo kwamba haoni haja ya kuendelea kuwepo Nou Camp. Msimamo wa staa huyo mwenye umri wa miaka 32 umekuwa mtihani mgumu kwa Rais wa klabu hiyo, Josep Maria Bartomeu, kwani ni majuzi tu mashabiki walipoanzisha maandamano ya kumtaka ajiuzulu. Bartomeu alimshawishi Messi akubali mkataba mpya mnamo 2017, lakini safari hii itakuwa vigumu iwapo atashindwa kumleta klabuni Neymar.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako