• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OLIMPIKI: Wadau wa Olimpiki wakemea hatua ya IOC kuiruhusu Tokyo kuendelea na maandalizi

    (GMT+08:00) 2020-03-19 08:57:29

    Waandaaji wa Olimpiki wameonywa kwamba wanaweka afya za wanariadha hatarini kwa kuendelea kuandaa michezo ya Olimpiki ya Tokyo na kwamba hakuna ufumbuzi bora wa kuendelea na Olimpiki. Michezo hiyo imepangwa kuanza Julai 24 licha ya michezo mingi kufutwa kutokana na mlipuko wa virusi vya korona. Bingwa wa olimpiki Katerina Stefanidi amesema Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC inahatarisha afya zao. Naye Katarina Johnson-Thompson wa Uingereza amesema hata kufanya mazoezi kwa sasa imekuwa ngumu na haiwezekani. Hata hivyo IOC imejibu kwa kusema kwamba hii ni hali maalumu inayohitaji ufumbuzi maalum. Kwa upande wa kocha maarufu wa riadha Renato Canova amesema kuendelea kufanya michezo hiyo ni sawa na kuwanyima wanariadha fursa sawa na za ushindani. Ameilaumu IOC na waandaaji wa Tokyo kwa kujali Zaidi vyombo vya habari na utangazaji na kusema hakuna olimpiki bila ya wachezaji. Canova amesema baada ya siku tatu Kenya inaweza kuwakataza wanariadha kukimbia kwa vikundi ili kuepusha kuenea kwa virusi hivyo, na kusema Olimpiki ya Tokyo ni lazima iahirishwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako