• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: TPL yaamua mechi kuchezwa bila mashabiki baada ya katazo la mwezi mmoja kuisha

    (GMT+08:00) 2020-03-19 08:58:13

    Bodi ya Ligi Tanzania (TPLBoard) imeweka maazimio manne ikiwamo ligi kuchezwa bila mashabiki baada ya siku 30 za kusimamishwa kwa mashindano yote nchini humo. Maazimio hayo yamefikiwa jana katika kikao cha Kamati ya uongozi na uendeshaji wa Ligi kilichofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotangaza kusitisha mikusanyiko ikiwemo matukio ya kimichezo nchini kwa mwezi mmoja. Ofisa Mtendaji wa Bodi (CEO), Almas Kasongo amesema katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Corona ulioingia nchini humo, wameazimia Ligi kuchezwa bila mashabiki itakapoendelea mwezi ujao. Alisema kingine walichoazimia ni Ligi kumalizika ndani ya mwezi Juni ili kutoa nafasi kwa timu zitakazoiwakilisha nchi kimataifa kuendelea na mchakato wa mashindano ya CAF. Alisema pia wao wataendelea kuwa maajenti wazuri kusimsamia afya kipindi hiki cha tahadhari ya Corona hivyo wameazimia Ligi ichezwe bila mashabiki mara itakapoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako